Wednesday, July 18, 2012

Maisha Lazima yasonge mbele! No matter what happens!




Nimejifunza  kwamba katika maisha hakuna tambarare,nikiwa na maana kwamba kuna vipindi mbalimbali katika maisha. Kuna kupanda na kushuka,kuna wakati wa kulia na kucheka. Ndio maana hata kwenye Biblia tunasoma katika Mithali 3:1 na kuendelea utaona, Kila jambo lina wakati wake. Hakuna wakati wa jambo moja tu siku zote. Inaanisha haiwezekani kuwa na shida tuu moja kwa moja, au raha tu moja kwa moja. Hakuna wakati wa kulia tuuuu au kucheka tuuuu…Nyakati katika maisha zinabadilika,hata hilo unalopitia sasa hivi litapita pia.

Nimejifunza  kwamba, haijalishi nini kinatokea katika maisha, au siku ni mbaya kiasi gani, lakini maisha lazima yasonge mbele na kesho yangu ni bora zaidi kuliko hali yangu ya leo. Nimejifunza kwamba haijalishi nampenda kwa kiasi gani mpenzi wangu au mtu aliye karibu yangu kwa kiasi gani kuna siku nitammiss tu atakapokuwa hayupo tena duniani. Nimejifunza kwamba katika maisha kuna fursa mbalimbali…,changamoto ni namna gani tunazitumia hizo fursa ili kututoa katika hali ya sasa na kutupeleka katika hali iliyo bora zaidi.
 
Nimejifunza kwamba kila wakati katika maisha nimezungukwa na maamuzi mbalimbali…..,changamoto ni kufanya maamuzi sahihi, wakati sahihi, mahali sahihi, kwa njia sahihi na kwa nia sahihi!
Nimejifunza kwamba watu wanaweza kusahau umesema nini, wanaweza pia wakasahau umefanya nini lakini ni ngumu kusahau ulivyofanya wajisikie/kujiona vipi! (Wajione bora au la, wajisikie vizuri au vibaya…wajione ni  wa muhimu au hawana…) How you made them feel!
 
Nimejifunza kwamba  bado nina mengi ya kujifunza katika maisha!
 Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
By. Mc. Hudson Kamoga – 0655 809091     

No comments:

Post a Comment